Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda hupoteza Trilioni 1.8 kila mwaka kutokana na utapiamlo:WFP

Uganda hupoteza Trilioni 1.8 kila mwaka kutokana na utapiamlo:WFP

Uganda imekuwa ikipoteza kiasi cha shilingi Trilioni 1.8 sawa na dola za Marekani Milioni 899 kila mwaka katika pato lake jumla la ndani kutokana na matatizo ya utapiamlo. Alice Kariuki anaarifu.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Utafiti huo uliendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya serikali ya Uganda, Kamishna ya mashirikino kwa maendeleo kwa bara la Afrika NEPAD, Kamishna ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa kwa afrika na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu WFP. Utafiti huo umefahamisha kuwa suala la ukosefu wa chakula haligusi pekee afya, bali ni suala linalohusu  hali ya uchumi pia.

Ikitumia takwimu ilizokusanya mwaka 2009, utafiti huo ulipima kiwango cha hasara ya kiuchumi ambayoUgandainapata kutokana na ukosefu wa lishe bora hasa katika maeneo ambayo yanaandamwa na utapiamlo kwa mara kwa mara. Utafiti huo umebainisha madhara yatokanayo kwa watoto kukosa lishe bora ni pamoja na kudumaa tatizo ambalo limetajwa kuwa ni matokeo ya ukosefu wa protein na vitamin wakati watoto hao wakiwa wangali matumboni mwa mama zao. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

 (SAUTI YA BYRS)