Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ziarani China, kukutana na Rais Xi Jinping kesho

Ban ziarani China, kukutana na Rais Xi Jinping kesho

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewasili nchiniChinaambako tayari ameshakuwa na mazungumzo na kundi la watendaji wa kampuni za kichina ambazo ni sehemu ya mtandao wa kampuni zinazoshirikiana na Umoja huo. Mazungumzoyaoyalijikita katika maendeleo endelevu na mabadiliko ya hali ya hewa. Habari zinasema kesho Bwana Ban atakutana na Rais Xi Jinping na waziri wa mamb ya nje Wang Yi. Halikadhalika atatembelea kituo cha mafunzo ya ulinzi wa amani karibu na mji mkuuBeijingambapo atazungumza kwa njia ya video na walinda amani waChinawalioko Sudan Kusini.