Wakimbizi waingia Cameroon na Niger kutokana na ukosefu wa Usalama Nigeria: UNHCR

18 Juni 2013

Wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa mbovu katika majimbo ya kaskazini mashariki mwaNigeria  ya Adamawa, Borno, na Yobe, ofisi za Shirika la Kuhudumia Wakmbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR zinaripoti kuwasili kwa wakimbizi zaidi nchiniNiger, na  sasa pia nchini Cameroon. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Nchini Cameroon, timu ya maafisa hao wa UNHCR walitembelea eneo ambalo lipo mpakani naNigeriaambako wamearifu kuwepo kiasi cha raia waNigeriawapatao 3,000. Raia hao walianza kukatisha mpaka na kuingia upande wa pili katika kipindi cha wiki iliyopita na inaelezwa kuwa kuwasili kwao kwenye eneo hilo ni hatua ya kunusuru maisha yao kutokana na msuguano unaendelea sasa baina ya serikali ya Nigeria na wanamgambo wa kundi la Boko Haram . Kiasi kikubwa cha wale waliowasili ni wanawake na watoto na wamekuwa wakipatiwa hifadhi kwenye makanisa na shuleni huku msaada mkubwa wa chakula wakitegemea kutoka kwa jamii inayowazunguka. UNHCR inasema kuwa imeanzisha juhudi kwa kushirikiana na mamlaka ili kuwapatia hifadhi salama na zenye viwango vya kuridhisha. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

 (SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 “Tayari tumetuma msaada wa dharura ambapo vyombo vyetu vimeondoka kutoka Niamey kuelekea Kusin Mashariki mwa jimbo la Diffa ambako zaidi ya watu 6,000 wamewasili wakitokea Kaskazini mwa Nigeria katika kipindi cha wiki zilizopita.Idadi hiyo inajumuisha wanageria 2,692 pamoja