Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa mabunge wahofia hali DRC: IPU

Muungano wa mabunge wahofia hali DRC: IPU

Muungano wa wabunge IPU umeelezea hisia zake kutokana na hatua ya kuharamisha kitu cha mbunge wa upinzani aliye kizuizini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ukihofia kuwa maisha yake yaneweza kuwa hatarini. Kiti cha Diomi Ndongala na vile vya wabunge wengine wanne nchini DRC viliharamishwa tarehe 15 mwezi huu baada ya kukosa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda mrefu.

Mungano wa wabunge unasema kuharamishwa huku kunaweza kusababisha mbunge huyo kukabiliwa mashataka mapya ya uasi ambayo yanaweza kuwa hukumu ya kifo ikiwa atapatikana na hatia. Jemini Pandya kutoka IPU anafafanua zaidi

(CLIP YA JEMIN PANDYA)