Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka serikali ya Uturuki na mashirika ya umma kutuliza misukosuko

Pillay aitaka serikali ya Uturuki na mashirika ya umma kutuliza misukosuko

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha uamuzi wa juma lililopita wa serikali Uturuki wa kusititisha hatua yoyote dhidi ya maandamano mjini Istabul hadi kutakapotolewa uamuzi wa mahakama na baadaye kupigwa kura ya maoni. Pillay ameishauri serikali ya Uturuki na mashirika ya umma kutumia njia ambazo hazitaleta misukosuko.

Pillay anasema kuwa bado hali si shwari na hatua za serikali za kukabiliana na maandamano zilisababisha kuwepo majeruhi wengi. Anasema kutokana na hatua za serikali mandamano yaliongezeka na kuzishirikisha pande zingine zikiwemo zinazohusika na haki za kibinadamu hasa haki za kukusanyika na kujieleza. Rupert Colvill kutoka ofisi hya haki za binadamu anafafanua zaidi.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)