Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yagawa msaada wa chakula kwa wakimbizi na wanaorejea Tissi, Chad

WFP yagawa msaada wa chakula kwa wakimbizi na wanaorejea Tissi, Chad

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema tangu mwezi Februari mwaka huu watu wamekuwa wakihama na kuvuka mpaka kutoka Sudan kuingia Chad kwenye mji wa Tissi jimbo la Sila.  Eneo hilo ni mahali ambako mipaka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan na Chad inakutana. Kufuatia kuongezeka kwa mapigano ya kikabila yanayoendelea katikati mwa Darfur na mapigano katika vijiji mbalimbali wakimbizi zaidi ya 30,000 na wanaorejea 26,000 wameripotiwa kukimbilia Mashariki mwaChadkwenye eneo la Tissi mwezi uliopita. Lengo la WFP huko Tissi ni kukidhi mahitaji ya wakimbizi, watu wasiojiweza, watoto na wanawake wenye utapiamlo na kuwasaidia kumudu matatizo yaliyopo. Idadi ya watu wanaosaidiwa na WFP nchini Chad tangu mwanzoni mwa mwaka 2013 ni 892,160.