Madhara ya ukame yanaweza kupunguzwa kwa kufuata sera madhubuti: Ban

17 Juni 2013

Katika siku ya kimataifa ya kutokomeza vitendo vyote ya kufanya dunia kuwa jangwa hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake na kusema licha ya kwamba ni vigumu kuepusha ukame lakini hatua za makusudi zaweza kuchukuliwa ili madhara yake yakapunguzwa. Bwana Ban amesema katika kipindi cha miaka 25 iliyopita dunia imekuwa hatarini kugeuka jangwa zaidi na vipindi vya ukame vimetabiriwa kusambaa zaidi na madhara yake kuwa makali kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Amesema ukame wa muda mrefu husababisha jangwa na matokeo yake ni hali duni za maisha na hata hatari ya mizozo ya jamii kwenye rasilimalikamavile maji na ardhi yenye rutuba. Hata hivyo amesema jambo la muhimu sasa ni kuondokana na mipango ya kushughulikia madhara ya ukame na badala yake kujenga mazingira ya kudhibiti ukame kwa kuzingatia mkutano wa kimataifa wa kisera kuhusu ukame uliofanyikaGenevamwezi Machi mwaka huu.  Ujumbe wa mwaka huu ni usiache mustakhbali wetu kukauka, na serikali yaTanzanianayo inaendelea na harakati za kulinda misitu ili kuepusha kugeuka jangwa kama anavyosema Frank Binagi Afisa misitu wa pori la akiba la Burigi mkoani Kagera.

(SAUTI YA BINAGI)