Ban alaani mashambulizi dhidi ya wanafunzi wa kike nchini Pakistan

17 Juni 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulizi yaliyolenga basi moja, hospitali na jumba la kihistoria nchini Pakistan ambapo watu 20 waliuawa wengi wakiwa ni wanafunzi wa kike. Kwenye taarifa kupitia kwa msemaji wake Ban amesema kuwa  ghasia dhidi ya wanawake zimeongezeka miaka ya hivi karibuni zikiwa na lengo la kuwazuia wasichana wasihudhurie masomo. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari bomu lililokuwa limefichwa kweye basi iliyokuwa ikiwasafirisha wanafunzi wa kike lililipuka kwenye mji waQuettana baadaye watu waliokuwa wamejihami wakavamia hospitali ambapo waathiriwa walikuwa wamepelekwa . Jumla ya watu ishirini waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter