Mnyarwanda kuongoza kikosi cha ujumbe wa UM nchini Mali

17 Juni 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Meja Jenerali Jean-Bosco Kazura kutokaRwandakuwa Kamanda wa kikosi cha ujumbe wa umoja huo cha kuweka utulivu nchiniMali, MINUSMA ulioundwa hivi karibuni. Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa jukumuhiloataanza tarehe Mosi mwezi ujao ambapo kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama, MINUSMA itapokea rasmi majukumu ya ujumbe wa usaidizi nchiniMaliuliokuwa ukiongozwa na Afrika, AFISMA. Meja Jenerali Kazura ana uzoefu wa miaka 24 wa masuala ya kijeshi kitaifa na kimataifa na kabla ya uteuzi huu alikuwa Kamanda wa Chuo cha Taifa cha mafunzo ya ulinzi nchini Rwanda na amewahi kuwa mshauri mwandamizi wa masuala ya kijeshi na usalama kwa Rais Paul Kagame kuanzia mwaka 2009 hadi 2010. Kamanda huyo  kikosi cha ujumbe wa MINUSMA ana shahada ya kwanza ya Kiingereza na Sayansi za jamii.