Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusiache mustakhbali wetu ukauke: UM

Tusiache mustakhbali wetu ukauke: UM

Leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza kuenea kwa jangwa ambapo ujumbe ni kwamba usiache mustakhbali wetu ukauke, ukijikita katika misitu ambayo ndiyo inategemewa kwa uhai wa sayari hii adhimu dunia. Harakati mbali mbali zinaendelea ikiwemo kuepusha watu kukata miti hovyo kwa ajili ya mikaa na kulinda maeneo ili yasitumike kukata magogo na kadhalika. Katika ripoti hii fupi George Njogopa kutoka Dar es salaam anamulika harakati za kudhibiti kuenea kwa jangwaTanzania.