Hali ya kibinadamu yazidi kuwa mbaya Yemen: UNICEF

17 Juni 2013

Hali ya kibinadamu nchini Yemen bado inasalia kuwa mbaya hata baada ya kupigwa kwa hatua za kuleta utulivu wa kisiAsa kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

UNICEF inasema kuwa Yemen inasalia kukumbwa na tatizo la uhaba wa chakula hali ambayo imechangia kewepo kwa utapiamlo na kukosa kukua kwa watoto. UNICEF inasema kuwa zaidi ya watoto 255,000 wanataabika kutokana na utapiamlo huku nusu ya wananchi wa Syria wakiwa hawa maji safi ya kunywa. Mjumbe wa UNICEF nchini Yemen Julien Harneis anasema kuwa mzozo wa sasa wa kisiasa nchini Syria umechangia kuongezeka kwa idadi ya watu walio maskini na idadi ya miundu mbinu iliyoharibiwa.

(SAUTI YA JULIEN HARNEIS)

”Hata kama hali mbaya ya mzozo wa tangu miaka miwili iliyopita imetoweka, uharibifu kwa miundo msingi kwa maisha ya watu bado imesalia. Kwenye eneo la Saada kuna karibu shule 230 zilizoharibiwa kabisa na hadi sasa hazijajengwa. Ugumu wa lishe nchini humo ni sehemu ya utapiamlo unaosabaishwa na mizozo ya kisiasa na ya kiuchumi na watu kukosa chakula kutokana na mzozo au ukosefu wa pesa, lakini pia utapiamlo na kukosa kukua. Na kwenye upande wa kukua karibu asilimia 58 ya nchi nzima haikui na ndiyo sehemu isiyokua zaidi duniani.”

Bwana Harneis anasema kuwa UNICEF inafahamu kuhusu karibu watoto 25 waliohukumiwa kifo nchini Yemen kwa makosa tofauti akiongeza kuwa UNICEF inafanya kazi na washirika kutaka kufanyiwa marekebisho adabu kwa mokosa yanayotendwa na watoto.