Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa misaada wako njiani kuelekea Kachin Myanamr:OCHA

Wafanyakazi wa misaada wako njiani kuelekea Kachin Myanamr:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limesema msafara wa malori 10 ya wafanyakazi wa misaada uko njiani kuelekea jimbo la Kachin nchini Myanmar.

Msafara huo una jumla ya watu 5100 ukiwa umesheheni vifaa vya kuokoa maisha ya watu vikiwemo ambavyo sio chakula. OCHA inasema hivi sasa fursa ya kuwafikia wanaohitaji msaada inatia moyo tangu kuzuka kwa machafuko Juni 2011 baina ya serikali na makundi ya waasi ambayo yamesababisha watu 100,000 kuzikimbia nyumba zao.

OCHA inasema mbali ya fursa kuwa ngumu kuwafikia walengwa pia shirika hilo lina matatizo ya fedha.