Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa uhamiaji kuanza Juni 18:IOM

Mkutano wa kimataifa wa uhamiaji kuanza Juni 18:IOM

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limesema kuanzia Jumatatu Ijayo Juni 18 litafanya mkutano wa kimataifa mjini Geneva kuhusu wahamiaji.

Kwa mujibu wa shirika hilo miongoni mwa ajenda kuu ni mchango wa wahamiaji hao katika mataifa waliyotoka. Imebainika kwamba wahamiaji hutuma nyumbani mambilioni ya dola kila mwaka.

Katika mkutano huo mawairi mbalimbali wanaohusika na jamii zao zilizoko ughaibuni watajadili masuala mbalimbali yanayowagusa wahamiaji ikiwemo ni yapi yamefanikiwa na yapi bado ni changamoto.