Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapata Rais mpya

14 Juni 2013

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapata Rais mpya

Uchaguzi umefanyika hii leo wa kumpata Rais wa kikao cha Sitini na Nane cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa naye ni Dokta John William Ashe kutoka Antigua na Barbuda. Grece Kaneiya na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GRACE)

Dkt. Ashe anashika wadhifa huo wakati huu ambapo Vuk Jeremic anahitimisha jukumu lake la kuongoza kikao cha 67 cha Baraza Kuu la Umoja wa Matafa. Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amemshukuru Bwana Jeremic kwa mchango wake katika kipindi chote hicho kuanzia mwaka jana huku akiahidi kushirikiana vyema na Rais Mteule wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu Dkt. Ashe katika kufanikisha ajenda mbali mbali ikiwemo hitimisho la malengo ya milenia na mipango na uendelezaji wa ajenda ya maendeleo baada ya 2015. Amemwelezea kama mtu makini na ambaye wana mtazamo wa pamoja thabiti kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.