IPU yaendelea kufuatilia kesi dhidi ya wabunge Burundi

14 Juni 2013

Umoja wa mabunge duniani, IPU unaendelea kushinikiza kupatiwa suluhu kwa kesi za madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi zinazokabili wabunge 20 na mbunge mmoja wa zamani kama anavyoripoti George Njogopa.(Taarifa ya George Njogopa)

Ujumbe huo ambao ni kamati ya Umoja wa Mabunge duniani unatazamiwa kuwasili nchini Burundi kuanzia june 17 na utasalia huko hadi june 20 ukiendesha tathmini namna utendaji kazi wa shughuli za mahakama dhidi ya wabunge kadhaa ikiwemo mbunge wa zamani Gerald Nkurunziza ambaye amekuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka mitano. Ujumbe huo pia utashughulikia suala la mwanasiasa mwandamizi Hussein Rajabu ambaye alihukumiwa kifungu cha miaka 13 jela. Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na utendaji kazi wa mahakama. Jemini Pandya ni msemaji wa IPU:

(SAUTI YA JEMIN PANDYA)