UM waitaka Belarus kuheshimu haki za binadamu.

14 Juni 2013

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya haki za binadamu nchini Belarus Miklos Haraszti, ameitaka nchi hiyo kutumia vyombo vyake kuhakikisha kwamba suala la haki za binadamu linaboreshwa.  Bwana Haraszti amesema kuwa mamlaka za dola pamoja na taasisi zake zimeendelea kubana haki za binadamu na wakati mwingine mamlaka hizo zinaweka ngumu wakati zinapotakiwa kumulikwa. Mtaalamu huyo amesema kuwa anaingiwa na wasiwasi namna taifahilolinavyoendelea kutekeleza vitendo ambavyo vinabinya haki za binadamu kwa kuweka sheria ambazo zinakwenda kinyumme na misingi ya kimataifa. Ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kurekebisha hali hiyo ili wananchi wake waweze kufurahia haki za binadamu.