Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM Imekamilisha tathimini ya maeneo yanayohifadhi wakimbizi Lebanon:

IOM Imekamilisha tathimini ya maeneo yanayohifadhi wakimbizi Lebanon:

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema limekamilisha tathimini ya haraka ya maeneo matano Kusini mwa Lebanon ambayo yanahifadhi wakimbizi toka Syria.Matokeo ya tathmini hiyo kwa mujibu wa IOM yanaashiria kwamba jamii za wakimbizi maeneo ya Saida na Sarafand yanahitaji msaada wa haraka ikiwemo malazi na vifaa visivyo chakula, huduma za afya, elimu ya usafi na miradi ya kuwaingizia kipato.