Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yakamilisha kuwahamisha wakimbizi wa Darfur kutoka kwenye mpaka na Chad:

UNHCR yakamilisha kuwahamisha wakimbizi wa Darfur kutoka kwenye mpaka na Chad:

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limemaliza zoezi la kuwahamisha wakimbizi wa Darfur kutoka katika eneo la machafuko la mpakani mwa Chad la Tissi.Wakimbizi hao wamepelekwa katika kambi mpya ya Ab Gadam ambayo sasa inahifadhi wakimbizi 10,247.

Mbali ya sababu za kiusalama zilizochangia pakubwa kuhamishwa kwa wakimbizi hao UNHCR inasema eneo la Tissi pia linakumbwa saana na hali mbaya ya hewa.