Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya dawa mpya kutibu Kifua Kikuu sugu, Tanzania yazungumza

Matumizi ya dawa mpya kutibu Kifua Kikuu sugu, Tanzania yazungumza

Shirika la afya duniani, WHO limetoa mwongozo mpya wa muda wa tiba dhidi ya Kifua Kikuu sugu, MDR-TB duniani. Lengo ni kupunguza muda wa tiba ikilinganishwa na sasa. Miongoni mwa nchi husika ni pamoja naTanzania. Je ni lini tiba mpya hiyo itaanza?. Dokta Blasbus Njako ni Kaimu Meneja Mradi wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini humo na katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa anazungumzia iwapo wana taarifa hizo mpya za matumizi ya Bedaquiline kutibu Kifua Kikuu sugu.