Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi kwenye mahakama kuu Kabul

Ban alaani shambulizi kwenye mahakama kuu Kabul

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-moon, amelaani vikali shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa mnamo Juni 11 mjini Kabul, karibu na jengo la mahakama kuu.Shambulizi hilo, ambalo wanamgambo wa Kitaliban wamedai kulitekeleza, liliwalenga raia, na hivyo kusababisha vifo vya yapata watu 17, na kuwajeruhi wengine 40.

Katibu Mkuu amesema mashambulizi yanayowalenga raia hayakubaliki, na yanakiuka sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Ametoa wito kwa wale wanaoyatekeleza mashambulizi kama hayo kukomesha mara moja vitendo hivyo vinavyoongeza mateso ya raia wa Afghanistan, na kutuma ujumbe wa rambirambi kwa familia za wahanga, huku akiwatakia walojeruhiwa nafuu haraka.