WHO yatoa muongozo wa matumizi ya dawa ya Bedaquiline kutibu Kifua Kikuu

13 Juni 2013

Shirika la afya duniani WHO linakadiria kwamba watu takribani nusu milioni wanaambukiwa ugonjwa sugu wa kifua kikuu kila mwaka na sasa imeamua kutoa muongozo wa muda wa dawa mpya ya kukabiliana na kifua kikuu sugu iitwayo Bedaquiline. Joshua Mmali na ripoti zaidi. (TAARIFA YA JOSHUA)

WHO inasema tiba ya sasa dhidi ya ugonjwa sugu wa kifua kikuu, MDR-TB ina changamoto kubwa ikiwemo muda mrefu wa tiba unaodumu kwa miezi 20 au zaidi ikihitaji mgonjwa kunywa dawa kila siku, dawa ambazo zinatia sumu mwilini na tiba si thabiti.

WHO yasema ni nusu tu ya wagonjwa wa kifua kikuu sugu ambao humaliza tiba kwa mafanikio hivyo basi imekuja na mwongozo wa dawa mpya kwa mujibu wa miongozo ya shirika hilo juu ya kifua kikuu sugu, iitwayo Bedaquiline ambayo inatibu kwa muda mfupi lakini ina masharti matano ambayo ni muhimu kuzingatiwa pindi itakapotumiwa kutibu watu wazima wenye kifua kikuu sugu.

Masharti hayo ni pamoja na ufuatiliaji wa mgonjwa na umakini kwa tiba hiyo kwa watu waishio na virusi vya ukimwi, wajawazito na wenye umri zaidi ya miaka 65.

Miongoni mwa nchi ambazo zimetajwa mpango huo kuanza niTanzania, Dokta Blasbus Njako ni Kaimu Meneja wa Mradi wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini humo, je wataanza kutumia Bedaquiline?

 (SAUTI YA Dkt. Njako)