Kuna uwiano katika masoko mengi ya chakula 2013/2014:FAO

13 Juni 2013

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema kwa mwaka huu wa 2013/2014 kuna uwiano katika masoko mengi ya chakula na hasa kwa upande wa nafaka. Hayo yamo kwenye ripoti ya mtazamo wa masoko ya chakula iliyotolewa Alhamisi. Grace Kaneiya anaripoti(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Ripoti hiyo ya FAO inasema kuwa, kiwango cha usafirishaji nje bidhaa za chakula katika kipindi cha mwaka 2013 kinakadiriwa kufikia dola za Marekani Trilioni 1.09, ikiwa ni karibu na kile kilichoshuhudiwa mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo kiwango cha mwaka huu kinazidiwa kwa asilimia 13 na kile kilichoshuhudiwa mwaka 2011 wakati kulipotolewa ripoti ya nusu mwaka.

Kuwepo kwa uzalishaji mwingi wa mazao katika nchi zinazoendelea, kipato cha chini kinachojitokeza katika nchi zinazokumbwa na tatizo la uhaba wa chakula kunatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zitakazofanya kushuhudiwe kiwango kidogo cha uagizaji wa bidhaa za nje