Mwakilishi mpya wa UNSOM awasili Hargeisa Somaliland:

13 Juni 2013

Mwakilishi maalumu mpya wa wa Katibu nchini Somalia bwana Nicholas Kay amewasili mjini Hargeisa, Somaliland Alhamisi ya leo na kukutana na Rais Ahmed Mahamed Mohamud (Silaanyo)  na maafisa wengine wa uongozi wa Somaliland. Hii ni ziara ya kwanza ya bwana Kay huko Somaliland tangu alipoanza majukumu yake kama mkuu wa mpango wa wa usaidizi wa Umoja wa MataifaSomalia(UNSOM) Juni 3.   

Alipowasili alipokelewa na wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa  Dr. Mohamed Abdillahi Omar, na kwa pamoja wakazuru makaburi ya pamoja Hargeisa, katika kuadhimisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliotendeka wakati wa uongozi wa Siyad Barre  kati ya mwaka  1984 na 1988.

Bwana Kay amesema amekwenda Somaliland kuwuhakikishia uongozi na watu wa eneohilokuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia  katika kudumisha amani na mafanikio ya baadaye.