Bila kuhusishwa mwanamke hakuna maendeleo ya anga za mbali:Tereshkova

13 Juni 2013

Hakuna maendeleo zaidi yatakayopatikana katika anga za mbali iwapo mwanamke hatoshirikishwa amesema Bi Valentina Treshkova katika kuadhimisha miaka 50 ya mwanamke kwenda anga za mbali. Flora Nducha anaripoti(Ripoti ya Flora Nducha)

Bi Tereshkova amesema hata ndege hawezi kuruka kwa bawa moja pekee na hivyo ndivyo kwa mpango wa anga za juu iwapo utaengua wanawake, basi uendelezaji zaidi wa mpango huo hautakuwa na mafanikio, hiyo ni kauli ya Valentina Tereshkova, mwanaanga wa kwanza wa kike kwenda anga za juu miaka Hamsini iliyopita.Katika safari hiyo ya kihistoria ndani ya ndani ya chombo Vostok 6, walizunguka dunia mara 48 kwa saa 70. Kuadhimisha miaka 50 tangu mwanamke wa kwanza aende anga za juu, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya anga za juu, UNOOSA imetangaza jopo la wanawake mashuhuri katika nyanja zihusianazo na anga za juu na Tereshkova anasema;