UNHCR yazindua kampeni maalum ya siku ya wakimbizi duniani.

13 Juni 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR, linazindua kampeni inayoonyesha madhara ya vita kenye familia iitwayo familia moja. Katika kutia nakshi kampeni hiyo wanamuziki mashuhuri kama vile Juanes kutoka Colombia, Lady Antebellum, Barbara Hendricks na mwanamitindo wa kimataifa Alek Khaled Hosseini pamoja na watu wengine nguli watashiriki katika kampeni hii kutoa wito kwa jamii kuchukua hatua. Kutokana na ongezeko kubwa la wakimbizi nchini Syria, Mali, Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kampeni hii inakumbusha uma kwamba waathirika wakuu wa vita ni familia nzima yaani baba,mama, na watoto. Katika kufikisha ujumbe nguli hawa wataandaa video maalum inayoonyesha jinsi vita vinavyoweza kubadili mustakabali wa familia kwa dakika moja na jinsi ambavyo wakimbizi wanaweza kusaidiwa na kupata tumaini hata katika nyakati ngumu. Wakizungumzia siku hiyo ya wakimbizi duniani mwanamuziki Lady Antebellum amesema wakimbizi wa Syria wanahitaji msaada ikizingatiwa kwamba mamilioni ya familia wamelazimika kukimbia makazi yao wakiwa na nguo pekee huku balozi mwema wa kudumu wa UNHCR Barbara Hendricks akisisitiza umuhimu wa dunia kushikamana kulinda familia dhidi ya vita amabavyo matokeo yake ni wakimbizi