Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Luteni Jenerali Babacar Gaye kuongoza BINUCA

Luteni Jenerali Babacar Gaye kuongoza BINUCA

Baada ya kuongoza kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC, MONUSCO, Luteni Jenerali Babacar Gaye kutokaSenegalsasa ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuwa Mwakilishi  wake huko jamhuri ya Afrika ya Kati.  Taarifa iliyotolewa New York, imesema Luteni Jenerali Gaye ambaye sasa ni msaidizi wa Katibu Mkuu katika masuala ya operesheni za ulinzi wa amani, ana uzoefu wa muda mrefu kwenye masuala ya diplomasia, siasa na kijeshi ndani ya Umoja wa Mataifa na kwenye serikali ya Senegal na ataongoza pia ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ujenzi wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, BINUCA. Luteni Jenerali Gaye ambaye ameshiriki pia shughuli kadhaa za ulinzi wa amani huko Iraq na Lebanon, anachukua nafasi iliyoachwa na Bi. Margaret Vogt kutokaNigeria, aliyemaliza muda wake.