Vikosi vya Mali na makundi ya waasi walikiuka haki za binadamu: UM
Umoja wa Mataifa umeorodhesha visa kadha vinavyokisiwa kukiuka haki za binadamu vilivyotekelezwa na wanajeshi nchiniMaliwakati wa oparesheni zao za kuwatimua waasi waliokuwa wamechukua udhibiti maneo ya kaskazini mwa nchi. Jason Nyakundi anaripoti.
(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)
Uchunguzi ulioendeshwea na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa umebainisha kuwa vikosi vya serikali viliendesha mauaji kwa misingi ya kikabila, vikahusika kwa kutoweka kwa watu , mateso na dhuluma za kila aina, kukakamatwa kwa watu na kuwazuilia. Naibu kamishna mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Flavia Pansieri ameliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa watoto wasichana waliolewa kwa lazima kwa wanachama wa makundi ya waasi kwenye miji ya Gao na Timbuktu na kudhulumiwa hasa kwa kubakwa. Bi Pansieri anasema kuwa kuna ripoti za kuingizwa kwa watoto kwenye makundi yaliyojihami kaskazini mwaMali.
(SAUTI YA BI PANSIERI)
“Walithibitisha pia visa vya mauaji yaliyo kinyume na sheria, kukamatwa kinyume na sheria na mateso, kutoweka kwa lazima na dhuluma za kingono kutoka kwa makundi yaliyojihami yalipodhibiti eneo la kaskazini mwa Mali. Ujumbe huo pia ulipokea malalamishi kutoka sehemu tofauti wakiwemo watu wa familia kuwa wasichana waliolewa kwa lazima kwa wanachama wa makundi yaliyojihami maeneo ya Gao na Timbuktu. Mara nyingi kuolewa huku kwa lazima kulisabaisha ubakaji kutoka kwa makudi hayo kati ya kipindi kisichozidi majuma mawili au matatu na kisha kurejeshwa kwa familia zao. Ni vigumu kubaini kiwango cha dhuluma za kimapenzi zilizofanyika nchini Mali mwaka 2012. Wanawake hawakutaka kuzungumzia dhuluma za kingono hadharani. Pia kumekuwa na ripoti za kutumiwa kwa watoto na makundi yote yaliyojihami kaskazini mwa Mali. Ripoti hizo pia zinasema kuwa ulipizaji kizazi kutoka kwa vikosi vya serikali na watu wa kawaida dhidi ya jamii za Tuareg na zile za kiarabu umepungua tangu mwezi Machi. Hata hivyo uwezekano wa ulipizaji kisasi dhidi ya jamii hizi umesalia kutoka na mahusiano yao na makundi ya waasi na hili linaweza kuwa kizingiti kwa wale waliokimbia makwao.”
Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linasema lina mipango ya kuteua mtaalamu wa haki za binadamu nchiniMali.