Umoja wa mataifa una wasiwasi na ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan Kusini
Hali ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini bado si nzuri wakati huu ambapo serikali inahaha kulinda raia dhidi ya vitendo vya ghasia, na hiyo ni kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kama anavyoelezea George Njogopa.(TAARIFA YA GEORGE)
Akizungumzia hali jumla ya mambo katika eneo hilo, Naibu Mkuu wa tume
ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Bi Flavia Pansieri amesema
kuwa baadhi ya vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu vimefanywa na
askari.
Amesema kuwa kuna hali ya kukatisha tama inayoendelea inayoendelea
kujitokeza na kwamba uhalifu zaidi umeshuhudiwa katika jimbo la
Jonglei lililopo mashariki mwa Sudan Kusin.
Katika ripoti yake kwa ofisi ya haki za binadamu Pansieri amesema kuwa
udhaifu wa vyombo vya haki na maamuzi kumesababisha kuwepo kwa
ongezeko kubwa la vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu .
Ripoti hiyo pia ilibainisha changamoto za kiusalama zinazoliandama
taifa hilo changa ambalo kwa miongo kadhaa liligubikwa na migogoro ya
wenyewe kwa wenyewe.
Akijibu kuhusu ripoti hiyo Waziri wa sheria wa Sudan Kusini John Luk
Jok amesema kuwa ni wajibu wa wananchi na vyombo vya dola kuheshimu
misingi inayozingatia haki za binadamu.