Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kwa Lugha ya Kiswahili yazinduliwa

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kwa Lugha ya Kiswahili yazinduliwa

 

Toleo la muhtasari wa ripoti ya maendeleo ya binadamu duniani imezinduliwa leo katika Chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya. Hii ni mara ya kwanza ripoti hii imechapishwa kwa lugha ya Kiswahili.

Lugha ya kiswahili inazungumzwa na zaidi ya watu milioni mia moja na hamsini, wengi wakiwa  katika eneo la Africa Mashariki, Afrika ya Kati na nchi za Afrika Kusini. "Kiswahili ni lugha muhimu sana haswa katika uwezo wake wa kuwasiliana na  wanyonge katika jamii, ikiwamo wanawake wa vijijini na vijana.

 Alisema Steven Ursino, Msimamizi wa UNDP nchini Kenya. “Kuweko kwa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kwa lugha ya Kiswahili itawasaidia wananchi kufahamu changamoto za maendeleo na kuwapa nafasi ya kutoa mchango wao ili kutatua matatizo yanayo wakabili.” Aliongezea kusema bwana Steven Ursino wakati akizindua ripoti hiyo.

Ripoti ya Maendelo ya Binadamu ya  mwanka wa 2013, ‘Kuinuka kwa Nchi za Kusini, Mandelo ya Biinadamu Katika Ulimwengu Anuwai.’ ilizinduliwa kimataifa mjini Mexico mwezi wa machi mwaka huu. Ripoti hii imechapishwa na shirika la maendelo la umoja wa mataifa na imetafsiriwa katika lugha zifuatazo;  Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, Kirusi na Kihispania, Kijerumani, Kihindi, Kijapani, na Kireno.

“Madhumuni ya ripoti ya maendeleo ya binadamu ni kuhusu kupanua uwezo wa binadamu kujiendeleza. Ni muhumu kwamba ripoti hii imechapishwa kwa lugha ambazo watu wanaelewa kwa urahisi. Tumefurahi sana kuongeza kiswahili kwa familia ya ripoti ya mandeleo ya binadamu.” alisema bwana Khalid Malik, mkurugenzi wa ofisi ya UNDP ya Ripoti ya Maendeleo.

Kiswahili ni lugha muhimu katika Afrika. Inatumika nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Visiwani  Comoro, Burundi Kongo na Msumbiji. Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika. Ripoti sasa imechapishwa kwa lugha 22 kwenye vitabu na tuvuti.