Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICTR kuendelea kuwasaka watuhumiwa wa mauaji

ICTR kuendelea kuwasaka watuhumiwa wa mauaji

Licha ya Mahakama ya kimataifa ya Rwanda ICTR iliyokuwa na makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania kumaliza muda wake watuhumiwa tisa wanaendelea kusakwa kwa garama yoyote ili kufikishwa mahakani.

Akongea na waandishi wa habari mjini New York , mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo Hasani Jallow amesema ICTR ambayo imewafungulia mashtaka jumla ya watuhumiwa 93 imekamilisha kazi za mashtaka na majukumu yake yatafanywa na mahakama ya kimataifa ya jinai nchini Ufaransa na kwamba kati ya watuhumiwa tisa ,sita kesi zao zimehamishiwa Rwanda kwa ajili ya kusikilizwa

Amesema kwa watuhumiwa vinara watatu ambao ni Felician Kabuga,Aporote Impiranya na Augustine Bizimana kesi zao zinashughulikiwa na mahakama ya kimataifa ya jinai ambayo ndiyo imechukua nafasi ya ICTR na itafanya kazi kupitia kupitia tawi lake lililoko mjini Arusha Tanzania lililoanza operesheni zake mwezi July mwaka

Amesema ni muhimu kwa watuhumiwa watoro wakakamatwa kwa ajili ya kuhakikisha amani katika ukanda wa maziwa makuu ambapo wengi wao wanatuhumiwa wamejificha huko.Amesisitiza nchi wanachama kushirikiana na mahakama hii ili kuwakamata watuhumiwa.

Akitoa wito kwa watuhumiwa hawa amesema

(SAUTI YA JALLOW)

"Kwa hawa waliotoroka ujumbe uko wazi hakuna ukomo wa muda kwa mashataka kwa kesi hizi ,kujificha hakusaidii na vyombo havitasita vitaendelea kuwasaka ,njia pekee waliyonayo ni kujisalimisha tu katika mchakato huu wa kimahakama ambao utaendeshwa kwa uwazi na uhurumjini Arusha ,laikini leo tunafurahi kwamba Umoja wa Mataifa na serikali zinahuisha ahadi zake katika mpango wa haki kwa kuendelea kuisaidia ICTR."