Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili Yemen

Baraza la usalama lajadili Yemen

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali nchiniYemen, wakati Ofisi ya kuratibu misaada ya kibindamu, OCHA ikisema idadi ya wakimbizi wa ndani nchini humo imepungua, kwa kiasi kikubwa. Joshua Mmali na taarifa zaidiTAARIFA YA JOSHUA

Yemenndiyo nchi pekee iloweza kujiibua kutoka kwenye machafuko na makubaliano yalotokana na mazungumzo ya amani, pamoja na kuweka barabara ya kina ya utaratibu wa kufuatwa na kipindi cha serikali ya kidemokrasia ya mpito. Hayo yamesemwa na Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusuYemen, Jamal Benomar, wakati akilihutumia Baraza la Usalama, ambalo limekutana kuhusu hali nchini humo.

Bwana Benomar amesema serikali na watu waYemenwanapaswa kupewa hongera kwa kuweka ahadi zao, licha ya changamto walizokumbana nazo wakati wa mazungumzo ya amani, huku akiwatolea mwito waendelee kwenye mkondo huo.

Amesema njia pekee ya kuendelea ni kupitia mazungumzo ya wazi na kuyatatua matatizo ya mfumo wa zamani

"Serikali bado haijatimiza wajibu wake wa kubuni tume ya uchunguzi katika matukio ya mwaka 2011, au kuweka sheria kuhusu haki katika kipindi cha mpito. Ni kupitia hatua muhimu kama hizi, ndipo Wayemeni wanaweza kuweka njia ya kufikia maridhiano ya kitaifa na Yemen mpya. Hali ya usalama bado ni tete katika maeneo fulani ya nchi. Licha ya juhudi zote za kukabiliana na Al-Qaeda katika rasi ya Arabia, bado ni tishio kubwa.

Wakati huo huo, Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema idadi ya wakimbizi wa ndani nchiniYemenimepungua tokea karibu elfu sabini hadi elfu sita tu.