Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Indonesia bado yakabiliwa na changamoto ya makazi bora

Indonesia bado yakabiliwa na changamoto ya makazi bora

Indonesia imetajwa kuwa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha kwamba inaendeleza na kulinda haki za kupata makazi bora miongoni mwa wananchi wake hali ambayo imesababishwa na ukuaji wa kasi wa miji na kukosekana kwa mipango endelevu. Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Raquel Rolnik amesema kuwa kutokana na hali hiyoIndonesiainakabiliwa na majanga ya kimazingira yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi . Hata hivyo ameeleza kuwa, taifahilobado lina fursa kubwa ya kurekebisha kasoro hizo na ameitaka kusukuma mbele agenda za kimaendeleo huku ikitilia mkazo udhibiti wa uongezeko holela la watu katika maeneo ya mijini. Bi  Rolnik alipewa jukumu la Baraza la Haki za binadamu la kutathimini na kukagua haki za kupata makazi bora nchini humo na kisha kutoa mapendekezo yake.