Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yamulika ajira ya vijana katika mkutano wa ILO

Tanzania yamulika ajira ya vijana katika mkutano wa ILO

Wakati mkutano mkuu wa 102 wa shirika la kazi duniani ILO ukiendelea mjini Geneva, Tanzania inatarajia kutumia mkutano huo kuimarisha ajira za vijana.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Mwakilishi wa serikali ya Tanzania Eric Shitindi amesema ajira kwa vijana ndio changamoto kuu na kwamba kupitia mkutano huo wanatarajia kujifunza na kupata mbinu mpya za kuzalisha ajira kwa vijana nchini humo.

(SAUTI SHITINDI