Mitaala ya shule ijenge utangamano baina ya makundi badala ya ubaguzi: Ruteere

11 Juni 2013

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki za watu wa kigeni na aina zingine za ubaguzi, Mutuma Ruteere amezungumzia nafasi ya elimu katika kutokomeza vitendo vya ubaguzi na chuki kwenye maeneo mbali mbali duniani. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.(Taarifa ya Assumpta)

Ni kwenye kikao cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea mjini Geneva, Uswisi ambako mtaalamu huyo Mutuma Ruteere amesema mzizi wa fitna hizo unaweza kung’olewa iwapo elimu itaanza kutolewa mashuleni tangu watoto wanapokuwa wadogo. Katika ripoti yake ya mwaka, mathalani amesema mitaala isijikite tu katika haki za binadamu bali pia michango mbali mbali kwenye jamii kutoka kwa makundi madogo ya kijamii, wahamiaji na wengineo ambao wako pembezoni. Amesema hatua hiyo ni muhimu ili mitaala isaidie kujenga utangamano na siyo kuonyesha watu wa kundi fulani rangi ni bora kuliko wengine.

(SAUTI YA RUTEERE)