Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yaomba dola milioni 40 kwa ukunga na dhuluma za kijinsia Syria

UNFPA yaomba dola milioni 40 kwa ukunga na dhuluma za kijinsia Syria

Shirika la Idadi ya Watu katika Umoja wa Mataifa, UNFPA, linajitahidi kuokoa maisha ya akina mama waja wazito kwa kutoa huduma zinazozuia vifo vya akina mama katika uzazi, pamoja na dhuluma za kijinsia kwa wakimbizi wa ndani na nje ya Syria. Joshua mmali na maelezo zaidi(RIPOTI YA JOSHUA MMALI)

UNFPA imesema, miongoni mwa idadi ya watu ambao wameathiriwa na mzozo nchini Syria, kuna wanawake 270,000 wajawazito na wanawake 64,000 nje ya Syria.

Shirika hilo limetoa ombi la dola milioni 40 kufadhili kazi yake nchini humo, hasa kukabiliana na visa vya dhuluma za kijinsia ndani na nje, ambazo zinahusisha ubakaji na aina nyingine za ukatili.

UNFPA inasema takriban wanawake 2,000 wamepokea msaada ndani mwa Syria, huku wengine 4,000 miongoni mwa wakimbizi nje ya Syria wakiwa wamepokea msaada unaohusiana na dhuluma za kijinsia.

Kwa mujibu wa UNFPA, uzazi kwa njia ya upasuaji umeongezeka kwani akina mama wengi wanachagua njia hiyo ili kuhakikisha wanahudumiwa na mkunga mwenye ujuzi tosha.