Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 90 ya wakimbizi wa ndani warejea makwao Yemen: OCHA

Asilimia 90 ya wakimbizi wa ndani warejea makwao Yemen: OCHA

Zaidi ya asilimia 90 ya wakimbizi wa ndani wamerejea kwenye jimbo la Abyan kusini mwaYemen baada ya kupungua kwa ghasia , kurejea kwa huduma na pia kufunguliwa kwa masoko. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA ni kwamba idadi ya wakimbizi wa ndani  kusini mwaYemenimepungua kutoka watu 68,533 mwezi Disemba mwaka uliopita hadi watu 6,133 mwezi Aprili mwaka huu. Hata hivyo wale wanaorudi makwao wanaishi kwenye nyumba zilizoharibiwa huku utawala wa maeneo hayo ukifanya jitihada za  kutoa huduma. Ombi la msaada wa kibinadamu kwa taifa laYemenni dola milioni 716 na hadi  sasa limefadhiliwa tu kwa asilimia 31.