Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msako wa Boko Haram wasababisha raia Elfu Sita kukimbia makazi yao Nigeria

Msako wa Boko Haram wasababisha raia Elfu Sita kukimbia makazi yao Nigeria

Nchini Nigeria zaidi ya watu Elfu Sita wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee wamekimbia makaziyaokaskazini mwa nchi hiyo na kuelekeaNigerkwa hofu ya usalama wao. Kulikoni, tujiunge na George Njogopa kwa maelezo zaidi.

(TAARIFA YA GEORGE)

Watu hao wameliambia shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kuwa wamelazimika kukimbia kwa hofu ya kukamatwa na serikali ambayo imeanzisha msako dhidi ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram. Vikosi vya serikali vinaendesha operesheni maalumu ya kuwasaka wanamgambo hao ambao wameweka ngomeyaokatika eneo la Kaskazini mwaNigeria, katika mji wa Baga ulioko karibu na mpaka naNiger. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

“Watu wameendelea kumiminika Niger ambako wametaja pia kuwepo kwa idadi kubwa ya wahalifu wanaorandaranda kwenye majimbo nchini Nigeria wakiwa na silaha.Kumekuwa pia na ongezeko kubwa la bei ya vyakula kulikosababishwa na uhaba jambo ambalo linazidisha hali ya wasiwasi. Wale wanaowasili wanakodi nyumba ama wanaishi na familia za wenyeji.Pamoja na kwamba wenyeji wameendelea kuonyesha moyo wa ukarimu lakini kuwepo kwa idadi ya wageni kunatia wasiwasi kuhusiana na uwezekano wa kukosekana huduma za maji na chakula. Niger inakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na ukame.UNHCR inapanga kusambaza baadhi ya bidhaa kwa wahamiaji wapya pamoja na wenyeji wao.”