UNHCR yahofia usalama wa raia waliokimbia mapigano Jonglei:

11 Juni 2013

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema lina shaka kubwa juu usalama wa raia waliokimbia makwao hukoJonglei,SudanKusini kutokana na mapigano yanayoendelea tangu mwezi Machi kati ya majeshi  ya serikali na vikundi vyenye silaha. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Maelfu ya raia wanaripotiwa kukimbia na kuwa wakimbizi wa ndani huko Jonglei, SudanKusini. Katika eneo la Pibor kumeshuhudiwa hali ya wasiwasi huku pia kukiwepo kwa vitendo vinavyofanywa kinyume cha sheria. UNHCR inasema maliza raia pamoja zimekuwa zikiharibiwa na hivyo kuzidisha hali ya wasiwasi kwa wananchi. Katika eneo hilola Pibor kiasi cha watu 148,000 wameathiriwa na hali yaona wengi wanaripotiwa kukosa makazi. Baadhi yaowameripotiwa kukimbilia maeneo ya porini ambako wanakabiliwa na hali ngumu  ya kimaisha.  Kumekuwa na ripoti pia baadhi ya wananchi wanalazimika kutembee mwendo mrefu kuelekea nchi za Kenya, Ethiopiana Ugandakwa ajili ya kuomba hifadhi ya kikimbizi. Shirika hilola kuhudumia wakimbizi linasema kukosekana kwa hali ya usalama pamoja na vikwazo  vya hapa na pale kumewafanya maafisa wake washindwe kufika kwa wakati kwa ajili ya kutoa huduma za usamaria mwema.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter