Nasikitishwa na jamii zinazonyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi: Ban

10 Juni 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza katika kikao cha Baraza Kuu cha kutathmini utekelezaji wa maazimio ya hatua thabiti dhidi ya ukimwi na utashi wa kisiasa dhidi ya ugonjwa huo ya mwaka 2011 na kusema kuwa miaka miwili baada ya tamko hilo bado kuna nchi ambazo zinaendeleza sera za unyanyapaa na  ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na Ukimwi na virusi vya Ukimwi.Amesemahiloni jambo linalomsikitishasanaakisema kuna mataifa 45 na maeneo ambayo bado yanazuia watu wenye virusi vya Ukimwi kuingia.

 (SAUTI YA BAN)

“Naendelea kutatizwa na kuenea kwa unyanyapaa, ubaguzi, ukatili wa kijinsia na sheria kandamizi dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wale waliohatarini kuambukizwa. Tatizo hili haliweza kutatuliwa kwa pesa zaidi. Tunapaswa kuongeza ujasiri na uadilifu kulinda wanajamii walio hatarini.”

 Katibu Mkuu akatoa ombi lake…

 (SAUTI BAN)

 “Tunapaswa kuhama kutoka kuwapatia dawa mamilioni ya watu na badala yake kuwapatia Mabilioni dawa za kupunguza makali ya Ukimwi kwani kwa kufanya hivyo kutakuwepo na mfumo thabiti wa afya unaoshughulikia matatizo ya jamii yake.