Serikali zawajibika kuchunguza na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake

10 Juni 2013

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake amesema serikali zinapaswa kuwajibika siyo tu kwa kuchunguza ukatili dhidi ya wanawake bali pia kwa kuwajibishwa kwa kushindwa kuzuia kutokea kwa vitendo hiyo.

Rashinda Manjoo akizungumza mjini Geneva, Uswisi amesema kuwajibishwa huko kunatokana na serikali kushindwa kudhibiti mifumo iliyopo inayofanywa zishindwe kuzuia ukatili dhidi ya wanawake.

Amesema serikali zinapaswa kuwawajibishwa wale wote wanaoshindwa kulinda haki za wanawake na au wanaoshindwa kuzuia vitendo vya ukatili na wale wanaotekeleza vitendo vinavyokiuka haki za wanawake.

Bi. Manjoo amesema kunatakiwa kuwepo kwa vigezo vya kufuata ambavyo vitatumika kupima iwapo serikali zinazingatia au la na kwamba serikali zina wajibu wa kuweka mifumo ya kutokomeza udhalilishaji wa wanawake.

Mifumo hiyo ni pamoja na kuhakikisha uchunguzi wa vitendo, kuwashtaki wahusika na kuahkikisha kuna mfumo wa kisheria unatoa haki kwa wahanga pamoja na jamaa zao wakati wa mchakato mzima wa kesi husika.