Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano London latoa matumaini ya vita dhidi ya kudumaa na lishe duni kwa watoto:

Kongamano London latoa matumaini ya vita dhidi ya kudumaa na lishe duni kwa watoto:

Kongamano lililofanyika London mwishoni mwa wiki kuhusu lishe kwa ukuaji limetoa fursa mpya ya kupunguza zaidi athari za kudumaa na mifumo mingine ya lishe duni kwa mamilioni ya watoto.

Hayo yamesema na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, likiongeza kuwa kwa watoto wanaokabiliwa na tishio lisilostahili la kudumaa, maradhi ambayo sio tuu yanawanyima afya ya kukuwa kawaida bali pia uwezo wa kusoma vyema, kupata kipato cha maana na kuchangia katika ukuaji wa jamii zao.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake kongamano hilo la London limebainisha ari ya kimataifa ya kukabili tishio hilo.

Kongamano hilo ambalo limewaleta pamoja viongozi kutoka mataifa mbalimbali, sekta binafsi na jumuiya za kijamii, limefadhiliwa na serikali za Brazilin a Uingereza pamoja na Children’s Investment Fund Foundation (CIFF).