Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yakaribisha ushirikiano wa Marekani na Uchina kudhibiti mabadiliko ya tabianchi

UNEP yakaribisha ushirikiano wa Marekani na Uchina kudhibiti mabadiliko ya tabianchi

Mkuu wa Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, Achim Steiner, amekaribisha uamuzi wa kuwepo ushirikiano kati ya Uchina na Marekani katika kukomesha matumizi ya aina ya fulani za kemikali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi .Bwana Steiner amesema tangazo la ushirikiano huo, ambalo limefanywa na Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Xi Jinping wa Uchina katika jimbo la California Marekani, huenda likawa ishara ya aya mpya ya ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Marais hao wawili walitangaza kuwa wataangazia aina fulani ya kemikali zinazoitwa HFC, zinazovusha gesi ya kaboni ambayo huharibu tabaka la Ozoni, ambalo huzuia miale mikali ya jua kuifikia ardhi.