Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikakati thabiti yahitajika kupunguza ukosefu wa usawa kama chanzo kikuu cha umaskini

Mikakati thabiti yahitajika kupunguza ukosefu wa usawa kama chanzo kikuu cha umaskini

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamepongeza utambuzi wa umuhimu wa usawa kama msingi wa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015, kama ilivyobainishwa kwenye ripoti muhimu ya Umoja wa Mataifa. Hata hivyo wametaka viongozi wa dunia kuridhia hatua madhubuti kutokomeza ukosefu wa usawa. Grace Kaneiya anafafanua zaidi.

 RIPOTI YA GRECE KANEIYA)

Wataalamu hao wanasema kuwa kupatikana kwa usawa si jambo la kupatikana kwa muujiza  lakini kupitia kwa kutekelezwa kwa malengo  kadha. Wanasema kuwa kundi la watu mashuhuri la Umoja wa Mataifa linasisitiza  uhusiano ulio kati ya ajenda mpya za maendeleo na kulinda haki za binadamu  kuhakikisha kuwa hakuna mtu hata kupitia kwa misingi ya kikabila , kijinsia na kijiogrofia anaweza kunyimwa haki zake za  binadamu na zile za kiuchumi. Ripoti hiyo inasema kuwa malengo ya maendelo yatatajwa kuwa yameafikiwa ikiwa yatafaidi pande zote  kwa jamii  na kuhakikisha kuwa maslahi ya jamii ndogo yameangaziwa. Wataalamu hao wanasema kuwa kujitolea huku kunahitajila kuwa na lengo la kuboresha mifumo ya kupunguza kutokuwepo usawa miongoni mwa wanawake , wanaume , watu maskini , matajiri na wale wanaoishi sehemu maskini na tajiri mijini.