Mkutano Dakar watathmini maendeleo ya haki ya chakula Afrika Magharibi

10 Juni 2013

Zaidi ya washiriki 40 wakiwemo wabunge, maafisa wa serikali na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiraia wanakutana Dakar, Senegal kuangalia mbinu bora za kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha kama haki ya binadamu. Jason Nyakundi na ripoti zaidi.

(TAARIFA YA JASON)

Mkutano huo ulioitishwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na chakula Olivier De Schutter na kundaliwa kwa ushirikiano na ofisi ya kamishina anayehusika na haki ya chakula pamoja na Shirika la Kilimo na Mazao la Umoja wa Mataifa FAO utawaleta pamoja waakilishi kutoka Benin, Burkina Faso , Ivory Coast, Ghana, Mali , Niger , Senegal na Togo. Mataifa ya Afrika MagharIbi yanakabiliwa na uhaba wa chakula wa mara kwa mara na athari za mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na misukosuko ya kisiasa. Mambokamahaya mara kwa mara yameuzuia serikali katika kuchukua hatua za kulinda watu kutokana na athari zake. Bwana De Schutter amasema kuwa ni muhimu kubuniwa kwa mipangilio ya kisheria kuhusu haki ya kuwa na chakula inayotambuliwa kimataifa  ili kuweka maslahi ya watu maskini , washikadau wadogo , wafugaji na wavuvi mongoni mwa ajenda za serikali.