UM wataka amani Benghazi

10 Juni 2013

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya UNSMIL umeelezea hali ya wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa mapigano yanayoukumba mji wa Benghazi na umetaka kurejeshwa kwa hali ya utulivu.

Watu kadhaa wameripotiwa kufariki duniani na wengine kujeruhiwa vibaya ikiwa ni matokeo ya machafuko yanayolikumba eneo hilo.

Katika taarifa yake, UNSMIL umetaka pande zinazohasimiana kujiepusha na matumizi ya nguvu za ziada na imeziomba pande hizo kukutana na kuanzisha majadiliano ya amani.

Duru za vyombo vya habari zimearifu kuwa kiasi cha watu 20 wamepoteza maisha na wengine 80 wamejeruhiwa wakati kulipojitokeza mapigano baina ya waandamanaji na askari katika mji wa Benghaz ambako ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya