UNICEF yabadili maisha ya mtoto Meshack

7 Juni 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Unicef kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limejikita katika kusaidia watoto na wakimbizi wenye ulemavu kwa ujumla ambapo wamebadilisha maisha ya baadhi ya wakimbizi wa ndani huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kutoa msaada uliowezesha kurejesha matumaini kwa walemavu hususani mtoto ambaye anamulikwa katika makala iliyoandaliwa na Joseph Msami

 

Ni Joseph Msami katika makala hiyo iliyomulika harakati za UNICEF na washirika katika kusaidia watu wenye ulemavu waliokimbia makazi yao kutokana na vita nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambao watoto wamepewa kipaumbele.

Mimi ni Alice Kariuki kwaheri kutoka New York