Baraza la Usalama lasikitishwa na hali mbaya Syria, lataka iruhusu watoa huduma.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameelezea kusikitishwa kwao na hali mbaya ya kibinadamu kufuatia mapigano makali ya hivi karibuni katika eneo la Al-Qusayr nchini Syria. Wajumbe hao wameitaka serikali ya Syriakuruhusu haraka na kwa usalama upatikanaji wa huduma za misaada stahiki ya kibinadamu ikiwamo kuwaruhusu wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuwafikia raia katika eneo hilowanaohitaji misaada haraka hususani matibabu. Pia wajumbe hao wamezitaka pande zote zinazozozana kufanya kila liwezekanalo kulinda raia huku wakiitaka serikali ya nchi hiyo kusimamia hilo. Baraza la usalama limesisitiza kwamba wote wanaokiuka sheria za kimataifa watakupambana na mkono wa sheria.