Mwaka mmoja baada ya mapigano ya kikabila Rakhine, bado wengi wanaishi ukimbizi: UNHCR

7 Juni 2013

Takribani Watu Laki Moja na Elfu Arobaini bado wamepoteza makaziyaohuko jimbo la Rakhine nchini Myanmmar ikiwa ni mwaka mmoja tangu ghasia za kikabila zisababishe vifo na maelfu kukimbia makwao. Taarifa ya George Njogopa inafafanua zaidi.(TAARIFA YA GEORGE)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa liko tayari kuipiga jeki serikali yaMyanmarili kufanikisha zoezi la kuwaandikisha wakimbizi hao wa ndani na wakati huo huo kuanzisha mchakato wa maridhiano ili raia hao waweze kurejea kwenye maeneoyaoya asili.

Hali ya sintofahamu katika jimbo la Rakhine ilianza kujitokeza kwa mara ya kwanza June mwaka uliopita kulipozuka mapigano  na kusababisha maafa kwa zaidi ya watu 75,000.

Kiasi cha watu 36,000 walipoteza makazi wakati kulipozuka machafuko mengine mwezi Octobakamaambavyo anavyofafanua msemaji wa UNHCR Adrian Edward

(SAUTI YA ADRIAN)