Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na washirika wake wahitaji dola Bilioni 5.2 kusaidia wananchi wa Syria

UM na washirika wake wahitaji dola Bilioni 5.2 kusaidia wananchi wa Syria

Umoja wa Mataifa na washirika wake wametangaza ombi la dola Bilioni Mbili nukta Tano, ombi ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa ajili ya wananchi wa Syria ambao bado wanakimbia makwao kutokana na mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa.Takwimu zaonyesha kuwa kwa wastani wasyria Elfu Saba wanakimbia nchi yao. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Mjini Geneva, Uswisi hii leo Umoja wa Mataifa na washirika wake wametoa ombi rasmi la dola bilioni Tano nukta Mbili kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Syria walio ndani na wale waliokimbia nchi yao kutokana na mapigano yanayoendelea.

Kati ya fedha hizo, dola Bilioni Nne nukta Nne ni kwa ajili ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ilhali dola Milioni 800 ni ombi la serikali za Lebanon na Jordan ambazo zinahifadhi wakimbizi wa Syria.

Msimamizi Mkuu wa misaada ya kibinadamu ndani ya Umoja wa Mataifa Valerie Amos amesema ombi hilo ni kwa mwaka huu wa 2013.

(SAUTI YA VALERIE)

Kwa mara nyingine tena Bi. Amos amesema lahitajika suluhisho la kisiasa kwenye mzozo huo wa Syria kwani misaada ya kibinadamu si suluhisho la kudumu wakati huu ambapo wasyria wanahoji kwa nini dunia imewatelekeza .