Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na sheria mpya za vyombo vya habari Burundi:

Ban asikitishwa na sheria mpya za vyombo vya habari Burundi:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesikitishwa kwamba sheria mpya ya vyombo vya habari Burundi  ina rasimu na mashariti ambayo yanaweza kuwa na athari mbaya kwenye uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Amesisitiza kwamba haki ya uhuru wa kujieleza na kuwa na vyombo huru vya habari ni kipengee muhimu katika kudumisha demokrasia.

Lakini sheria hiyo mpya inasemaje? Ramadan Kibuga ni mwandishi wetu nchini Burundi

 (SAUTI YA KIBUGA)

Katibu Mkuu ameitaka serikali ya Burundi kuhakikisha kwamba mfumo wake wa saheria unakwenda sambamba na desturi ya demokrasia nchini humo pamoja na viwango na sheria za kimataifa za haki za binadamu.